Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi linatarajia kufanya Kongamano la pili la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi tarehe 10 Juni 2017 Mjini Dodoma katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango na kuhudhuriwa na wadau wasiopungua 300 kutoka kwenye sekta ya Umma na Binafsi nchini.

Kongamano la mwaka huu litabeba ujumbe wa ‘Wezesha Watanzania kushiriki katika Uchumi wa viwanda ‘’.

Lengo la kongamano hili la siku moja ni kukutanisha wadau wa sekta ya Umma na Binafsi kujadiliana masuala ya uwezeshaji kiuchumi, kujifunza toka kwa wadau wengine namna ya kuchochea juhudi za uwezeshaji wananchi kiuchumi na kutambua  Taasisi za Umma na Binafsi nchini zilizofanya vizuri katika kuratibu masuala ya uwezeshaji katika maeneo yao.

Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB).

 

                           IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO KWA UMMA