Prime Minister's Office

Maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi

English
Body: 

Maonesho haya yatashirikisha Mifuko yote ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa lengo
la kutoa elimu kwa umma juu ya huduma mbali mbali zitolewazo na Mifuko hii. Aidha
katika Maonesho haya wajasiriamali katika Sekta mbalimbali walionufaika kupitia Mifuko
hii watashiriki ili kuonyesha matokeo ya uwezeshaji wao.

Mifuko itakayoshiriki ni Mfuko wa Kuendeleza Wajasirimali Wananchi, Mfuko wa
Uwezeshaji wa Mwananchi, Mfuko wa Pembejeo za Kilimo, Mfuko wa Maendeleo ya
Vijana, Mfuko wa Dhamana za Mikopo kwa Wajasiriamali wadogo na wa kati, Mfuko wa
Dhamana za Mikopo kwa Mauzo ya Nje ya Nchi.

Mifuko mingine ni Mfuko wa kuwasaidia Makandarasi, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii,
Mfuko wa Misitu Tanzania, SELF Microfinance Fund na PASS Trust Fund.
Wananchi wote wanaalikwa kuhudhuria Maonesho haya ili waweze kujifunza huduma
mbali mbali za Mifuko ya Uwezeshaji Nchini na namna ya kufaidika na huduma zake.
Maonesho haya yatafunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mh Kassim Majaliwa (MB), tarehe 18 Aprili, 2017.

Kauli mbiu ya Maonesho haya ni “WEZESHA WANANCHI KIUCHUMI ILI KUJENGA
UCHUMI WA KATI NA TANZANIA YA VIWANDA”

From: 
Tuesday, April 18, 2017 - 08:00
To: 
Saturday, April 22, 2017 - 16:00
Location: 
Dodoma katika Viwanja vya Mashujaa
Date Created: 
Tuesday, April 4, 2017 - 09:45
Last Updated: 
Tuesday, April 4, 2017 - 09:45