Habari

Imewekwa: Nov, 14 2018

TAARIFA KWA UMMA - UZINDUZI WA KITUO CHA PAMOJA CHA UWEZESHAJI

News Images

Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Shinyanga kupitia Halmashuri ya Mji wa Kahama linapenda kuchukua fursa hii kuwatangazia Wajasiriamali na Wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga juu ya uzinduzi wa kituo cha pamoja cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (Economic Empowerement One Stop Center) utakaofanyika tarehe 18 Novemba 2018 saa 2:00 asubuhi.

Kituo hicho kilichopo kata ya Nyihogo,Barabara ya Tabora kitazinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Jenista Mhagama (Mb) na kuanza kuhudumia Wajasiriamali baada ya ufunguzi.

Lengo la kituo ni kusaidia upatikanaji wa huduma za uwezeshaji za pamoja kwa wajasiriamali zikiwemo urasimishaji wa biashara, ushauri wa kibiashara,elimu na mafunzo ya ujasiriamali, upatikanaji wa mitaji na masoko, teknolojia na ufundi, hifadhi za jamii na afya, na uanzishwaji wa vikundi na vyama vya ushirika vya Akiba na Mikopo n.k.

Uanzishwaji wa kituo hiki ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kasimu M. Majaliwa (Mb)baadakutambua mchango wa Uongozi wa Serikali yaMkoa wa Shinyanga hususani Halmashuri ya Mji wa Kahama kuchukua jitihada ya kutenga na kugawa maeneo kwa Wajasirmali.

Kituo hiki ni muendelezo wa jitihada za Serikali katika kusogeza huduma muhimu za Kiuchumi kwa wananchi na kuchochea maendeleo ya viwanda hapa nchini.

Imetolewa na

Katibu Mtendaji,

Bibi Beng’i Issa.