Habari

Imewekwa: May, 24 2019

Fursa zitokanazo na mradi wa kufua umeme wa mto Rufiji kwa wafanyabiashara.

News Images

Tarehe 12 Desemba 2018, Serikali ya Tanzania ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ilitia saini makubaliano ya kutekeleza ujenzi wa mtambo wa kufua umeme utokanayo na maporomoko ya mto Rufiji, uliopo katika hifadhi ya wanyama ya Selous uliyopo kusini magharibi mwa Tanzania.

Mradi huo wa unakadiriwa kuwa na thamani ya Dolla za kimarekani bilioni 2.9 uliwekwa saini na Dkt. Tito E. Mwinuka, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kwa niaba ya Waziri wa Nishati, na Ahmed Sadek Elsewedy, Mkurugenzi Mtendaji wa Elsewedy Electric, na Mohamed Mohsen Salaheldin Mwenyekiti wa wakandarasi kutoka urabuni (Arab Contractors), makubaliana hayo yaliainisha kwamba mkampuni hayo mawili yangetekeleza ujenzi wa mradi kupitia ubia (Joint Venture).

Mtambo wa kufua umeme kupitia maporomoko ya maji wa mto Rufiji unatarajia kukamilika ndani ya miezi 42 tangu pale mkataba ulipoingiwa, na unategemewa kuzalisha MW 2,115 mpaka ifikapo Aprili 2022. Pia mradi huo wa kufua umeme utaambatana na ujenzi wa kituo cha kupooza na kusambaza umeme wa KV 400 zitakazo unganishwa katika gridi ya taifa ya umeme. Mradi huu mkubwa utatekelezwa na fedha za serikali ya Tanzania.

TPSF inapongeza serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais ya Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, kwa uthubutu wa kutekeleza mradi huu mkubwa wamaendeleo, kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya umeme kupitia maporomoka ya mto Rufiji. Sekta binafsi inaamini kuptia upatikanaji wa nishati ya umeme itachochea ajenda ya Serikali ya uchumi wa viwanda kuelekea katika utekelezaji wa Dira ya Tanzania ya Maendeleo 2025, inayokusudiakuifikisha Tanzania kuwamiongoni wa nchi zenye kipato cha kati (Middle income country)..

Katika kutekeleza wajibu wake na kuhakikisha Sekta Binafsi na wafanyabiashara nchini hawaachwi nyuma na wanashiriki kikamilifu katika fursa zote zinazotokana na mradi huu mkubwa, TPSF kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji la Wananchi Kiuchumi (NEEC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (EWURA) wameandaa semina kwa wadau itakayofanyika Dar es Salaam tarehe 11 mwezi wa sita 2019.

Semina hii inatarajia kuongeza ufahamu wa wadau kwenye mradi na fursa zilizopo. Semina hii pia itahudhuriwa na wakadarasi kutoka Misri wanaotekeleza mradi huo pamoja na timu ya usimamizi kutoka TANESCO wanaosimimaia utekelezaji wa mradi huo na wanatarajia kutoa mawasilisho (Presentation) kwa wadau watakaohudhuria.

Mategemeo na malengo makubwa yanatarajiwa kutoka kwenye semina ni:

Kuwafahamisha watanania juu ya fursa zinazotokana na mradi huu, haswa aina ya vifaa na bidhaa zitakazohitajika kutoka nchini.

Kuwataarifu wafanyabiashara ambao wanahamu ya kushiriki katika minyororo ya thamani mbalimbali na kuwapatia ujuzi pamoja na nyenzo zitakazowawezesha kushiriki kikamilifu kwenye mradi.

Kuwasikiliza wakandarasi kutoka Misri juu ya mpango wao wa kushirikisha wazawa katika utekelezaji wa mradi huu, pamoja na kuwapanga wazawa waweze kushiriki kikamilifu.

Kuwasikiliza wahusika wa mradi juu ya utaratibu amabao wazawa wanaweza kushiriki katika zabuni mbalimbali. Pia, kufahamau aina ya makampuni na sekta mbalimbali ikiwemo ya watoa huduma watakaohitajika katika kutekeleza mmradi huu ma bilioni.

Tunatoawito kwawafanyabiashara wote na wadau wote ambao wanahamu na madhumuni kushirki kwenye mradi huu mkubwa wa maendeleo nchini, wajiandikishe kabla ya semina kujihakikishia ushiriki kupitia tovuti ya TPSF au barua pepe events@tpsftz.org.